"Nusura,heri tukimbilie ugani kunako vichako." Nilimsihi mbasi wangu ambaye alikuwa keshaelekeza dira yake upande wa vyumba vya malazi.Kila mtu alikuwa akisharidi.Roho mkononi,pumzi mbilimbili.Mimi hapa,kifua kilikuwa kikinipanda na kunishuka ja ngalawa ipambanavyo na mawimbi baharini msimu wa upepo wa tufani.Kisha tukasikia milio ikialika.Moshi mweusi tititi mithili ya kizimwili ulikwa ukipaa angani.Baina yetu hakuna aliyejua ikiwa ilikuwa milio ya risasi au mialiko ya vitoa machozi.Kwa mbali ,niliweza kuwaona wafalme na mabuti yao ya chuma wakikimbia marshimarshi kuelekea tulikokuwa.Uwanjani tulikokimbilia tuliweza kuona yaliyokuwa yakiendelea.Nilizidi kujisogeza ukingoni mwa uchanjaa kwa hofu na hawafu ya kuonekana.Hamkani niliyokuwa nayo iliipiku ile ya farasi matege aliyepelekwa kwenye mashindano ya mbio huku akiwa na mguu kiguru kwa mpigo.Walioniita mwoga niliwacheka kimoyomoyo.Walikosa kuing'amua siri iliyofichama kuwa kwa shujaa kungeenda kilio....
Wale waliokuwa wamekimbilia usalama wao vyumba vya kulalia ndio walioonyeshwa ving'irimoto bin vimondo.Bila shaka waliyaalani matumbo yaliowazaa.Ushawahi kukiona kifo kwa maozi yako mawili?
Basi hicho ndicho walichoonyeshwa.Walipewa kichapo cha kelbu aliyebaua msiktini.Yakini walihuzunisha kwa mvua ya viboko iliyowanyeshea.Ile ya mtego wa panya kunasa waliomo na wasiokuwemo nafikiri ilisadifia hapa.Hawakutaka kujua ulikuwa mhusika au la.Lao muhimu ilikuwa ni wakupate tu...wakuonyeshe kilichomfanya sangara bkuchomwa moto.Watu wengi walitamani lau ardhi ifanye ufa iwahifadhi kwa kuwadidimiza wazima wazima .Lakini wapi?Ikiwa hazikuwa ndoto za panya kumfunga paka kengele basi zilikuwa zile za Alinacha.
Waliopatikana walipigwa kibobo.Nakumbuka hata mmoja aliyekuwa akitiririkwa na ngeu mwili mzima.Kunaye asaa aliyevunjwa fupaja kenyekenye na kuachwa akichechemea kama kiguru.Ila cha kustaajabisha ni roho ya mauko!.Ili kuitetea nafsi yake lemavu alijikusuru kutimua mbio za ajabu kiasi cha kwamba aliweza kuibuka kidedea kwa kuwashinda hata wale waliokuwa na miguu
salama.Ikrari,kiserema hujalima kikashinda jembe zima.Walionaswa walipitia tajriba ya kipigo ambacho kumbukumbu yake ilibakia katika taamuli ya nadhari zao miaka na dahari.Kuna waliopiga kwenzi za vilio vya shake na majonzi ja chozi la mliwa.Nani awasikie?Kilio kisaidie nini?Pukachaka!Kilio si dawa.
salama.Ikrari,kiserema hujalima kikashinda jembe zima.Walionaswa walipitia tajriba ya kipigo ambacho kumbukumbu yake ilibakia katika taamuli ya nadhari zao miaka na dahari.Kuna waliopiga kwenzi za vilio vya shake na majonzi ja chozi la mliwa.Nani awasikie?Kilio kisaidie nini?Pukachaka!Kilio si dawa.
Ghafla bin sadfa,kule uwanjani tulikojifichia tuliona karandinga ikija shoti.Haraka ya umeme ikiwa mshale ulikuwa polepole.Mitutu yao tayari walikuwa keshaielekeza kwetu ange kufyatua.Masalaaale!Nani abakie!Nilichana mbuga nambari mguu niponye visigino vikagusana na kisogo.Tulipoteleana mimi na mabui wangu.Nilijikuta katikati ya msitu wa mishajari ya miiba.Kila upande nilioangalia kulikuwa malindi yaliyokuwa na giza totoro.Nyuma nako hakukurudika.,niliona vumbi likitifuliwa tifu tifu.Ni sahali wale mabwana walikuwa wakitufuata nyuma.Huko mbele nilipokuwa niking'ang'ana kukutu kutoka kupitia mwanya mdogo kwenye ua wa chuo ndipo nilipokutana na Nusura.Akanisukuma nitoke ili naye atumie kipenyenye chicho hicho kujinusurisha pia.
Nje tulikotoka,tulitimua mbio kuokoa maisha yetu huku tukihema ja kelbu aliyenusurika kumezwa na chatu.Tukakutana na kaumu ya wenzetu ambao walikuwa wamehamanika upeo wa kuhamanika.Tukakimbia pamoja.Tulikuwa bimithi vipofu wengi walioongozana njia ilhali wote hawakuwa wakiona.Lengo letu lilikuwa almuradi tujinasue.Sote hatukuzijua janibu zile.Zilikuwa ngeni kwetu.Tulivurumiza na kufululiza tu bila mwelekeo.Muradi kuepukana na mazingira yale fishi kwani hata duru ziliarifu kuwa vitongoji vile aghalabu vilistakimiwa na shumdwa ambao waliripotiwa mara kwa mara kuwafarakanisha watu na sayari ya tatu.Tulijawa na wasiwasi wa waasi walioasi.
Nje tulikotoka,tulitimua mbio kuokoa maisha yetu huku tukihema ja kelbu aliyenusurika kumezwa na chatu.Tukakutana na kaumu ya wenzetu ambao walikuwa wamehamanika upeo wa kuhamanika.Tukakimbia pamoja.Tulikuwa bimithi vipofu wengi walioongozana njia ilhali wote hawakuwa wakiona.Lengo letu lilikuwa almuradi tujinasue.Sote hatukuzijua janibu zile.Zilikuwa ngeni kwetu.Tulivurumiza na kufululiza tu bila mwelekeo.Muradi kuepukana na mazingira yale fishi kwani hata duru ziliarifu kuwa vitongoji vile aghalabu vilistakimiwa na shumdwa ambao waliripotiwa mara kwa mara kuwafarakanisha watu na sayari ya tatu.Tulijawa na wasiwasi wa waasi walioasi.
Kwa sababu ya kukimbia sana, nilikuwa nimechoka tiki!Nadhani hata mdudu chungu angalinibwaga ikiwa angalitua popote juu ya kiwiliwili changu.Upepo mwepesi tu ungenipiga dhoruba kuniangusha chini pu!Kutazama nyuma!Walikuwa bado wakituandama.Tungefanyaje na kila mmoja wetu alikuwa amechoka?Tukaamua kupumzika."Vile nnavyojihisi sidhani ikiwa ninauwezo wa kukimbia tena.Ahhh!Kama wanakuja nawaje.Siwezi tena kukimbia."Mmoja katika ile kaumu yetu alilalamika.Mara rununu yangu ikakereza "ngrrrrrr!Ngrrrrrrr!"mwanafunzi mwenza alikuwa akinipigia.Simu tamba ilitoa ilani kuwa kiwango cha nishati kilikuwa chini na ingezima muda mchache baadaye.Nilifanikiwa kupokea taarifa kutongoa mawili matatu na aliyenipigia."Wame.....tup..atia nusu saa tube..be vi..ra..go vyetu...."Simu ikakatika.Nilipojaribu kumpigia."samahani mteja wa nambari unayopiga hapatikani kwa sasa"Lahaula!.Kisha simu yangu ikazimika kabisa.Mmoja wetu naye alipokea simu akiarifiwa kuwa chuo kilikuwa kimefungwa bila tarifa za kufunguliwa kwake.Wanagenzi walikuwa wamepewa nusu saa tu kukusanya virago vyao kupahama chuoni ila kabla kuchukua mizigo yako wewe mwanafunzi mnyonge ilikubidi kuadhibiwa kwanza na wanajeshi wa FFU almarufu Fanya Fujo Uone.Swali je,tungerudi vipi mahali pa tenge tahanani kama pale?Mie binafsi, nilikuwa nimeacha kitambulisho changu huko chuoni.Kwa sababu ya kudora kwa usalama katika hara ile ilikuwa vigumu kutembea bila kitambulisho.Askari polisi walikuwa wakifanya misako na kuwashika waliokosa vitambulisho.Tayari shinikizo la fikra likaanza kunifanya kichwa kuniwanga.Rasi yangu ilikuwa nzito falaula habta.Kuuchoma msumari wa moto juu ya donda aidha vyeti vyangu vyote vya kimasomo nilikuwa nimeviacha chuoni.Mshipa wa tumbojoto na jakamoyo ulinipiga vibaya huku mtima ukinipapa.Kidari na suduri vilinitika na kunituturika tik-tak tik-tak ja saa kweche.
Hatimaye tukala yamini,liwalo naliwe kufa gari kufa dereva."Turudi..wakiamua kutunyonga itakuwa ni heri ya Mola pia.Kila mja ataonja mauti ati!"Nilivunja ukimya wa maziarani uliokuwa umeshamiri tulipokuwa tukipumzika.Tukaanza safari ya kurudia nyayo zetu.Kumbe mbio za sakafuni huishia ukingoni!Tuliruka kiambaza kuingia chuoni.Hatukutumia lango kuu kwani tulijua tungenaswa na kupewa adhabu kali zaidi.Tulipoingia sote,tulinyapanyapa kama simba marara aliyenyemelea windo lake.Tulipofika karibu,walikuwa wameshatuona kwa mbali.Amri ikamtoka mmoja wao"kila mtu mikono juu..."mwingine aliyekuwa na sauti ya zenengo akadakia,"wewe shika masikio...kwa nini unaweka mikono juu?"Zumbukuku...lala chali na upige mbizi ardhini... leo mtachunua nyuso zenu"Waliochelewa kutii amri walishtukia mikwaju na mateke vikiwaingia pasi simile!Si kubobotwa na kunyukwa makofi huko!Kila mtu alikuwa amefyata mdomo kama bendera shwarini maji mtungini.Nani?nani angeweza kufurukuta mbele ya unyago wa bomba?Nani angechezea mkareti umpapure?Hmmmmm!Angurumapo simba mcheza ni nani?
Sote tulikuwa tutwe hatuna hatunani tuungwapo hatuungami ungedhani tumekumbwa kilingeni."Churachura mpaka mnakolala ...mchukue masanduku yenu.ukichukua shanta lako uyaone paa majengo ya chuo hiki mpaka utakapotaarifiwa.Haraka!"Walizidi kuamrisha.Maskini!Sasa nilikuwa nimeshindwa kuhimili uzito wa kiwiliwili changu.Mafuti yangu yalishasalimu amri ya kuupweteka mwili wangu chini ila nilijitahidi na kujikaza kisabuni kufa king'onzi."Unataka kumwangukia nani? inuga ugibie na uziagalie juba"Alinitisha mwanajeshi mmoja kwa lafudhi ya lugha yake.
Sote tulikuwa tutwe hatuna hatunani tuungwapo hatuungami ungedhani tumekumbwa kilingeni."Churachura mpaka mnakolala ...mchukue masanduku yenu.ukichukua shanta lako uyaone paa majengo ya chuo hiki mpaka utakapotaarifiwa.Haraka!"Walizidi kuamrisha.Maskini!Sasa nilikuwa nimeshindwa kuhimili uzito wa kiwiliwili changu.Mafuti yangu yalishasalimu amri ya kuupweteka mwili wangu chini ila nilijitahidi na kujikaza kisabuni kufa king'onzi."Unataka kumwangukia nani? inuga ugibie na uziagalie juba"Alinitisha mwanajeshi mmoja kwa lafudhi ya lugha yake.
Nilishajiika.Nguvu zilizokuwa zimenitindika zilinijaa pomoni ghafla,nikajaribu kadri ya uwezo wangu kujinasua hadi chumba cha malazi.Mwili wangu ulikuwa ukinipwita.Uchovu ulizidishwa hasa nilipovipanda vidato hadi orofa ya sita ambako ndiko chumba chetu mimi na rafiki yangu Nusura kilikokuwa.Jengo hilo refu la ghorofa halikuwa na kambarau.Ilitubidi kujikakamua kukwea ngazi,waama lisilobudi hutendwa.Kuvipanda vidaraja nayo ilikuwa kazi ya kivyake.Nilipowasili chumbani nilichukua kigudulia cha maji nikayagugumia ndipo nimuone Nusura akitweta kama kwamba alitaka kuzimia.Nilimpa maji yaliyokuwa yamesalia hivyobasi akarudi katika hali yake ya kawaida.Bila ya kupoteza wasaa, tulichukua makasha yetu japo kwa shaghalabaghala na kuteremka vidato tukielekea lango kuu.
Pambizoni mwa baraste,wanajeshi wa FFU walikuwa ange wameshika doria.Tulimuomba Mterehemezi atuepushe na rangaito hili.Niliomba dua kumpigia ukemi wa kuomba msaada kwa Muumba wangu.Taib!Zindiko la mwoga ni ukemi.Vitu vya wanagenzi wenza vilitapanyika tarikini.Wenyewe walihofia kuviokota ndipo wakaviacha.Kijasho chembamba kilitutiririka tiriri ;bwaibwai kwa jekejeke tulilokuwa nalo.
Tulipokuwa tukisubiri basi ili tusafiri kwenda kwetu Njooni ndipo nadhari mwafaka ya chanzo cha matukio haya iliponijia.
Asasi yake hasa ilikuwa ni kupigania haki.Chuoni hapakuwa na tarakilishi na zile kiduchu zilizopatikana nazo hazikuwa zimeunganishwa na mtandao wa utandabui wa utandawazi wa elimu.Maktabani nako, viada vilikuwa vichache mno.Hali duni ya miundomsingi chuoni nalo lilikuwa tatizo jingine tata ,kitendawili kigumu kilichokosa mteguzi.Kwa mujibu wa idadi ya wanagenzi na vifaa vya masomo vilivyokuwepo.Kulikuwa na nakisi kubwa sana ya vifaa vilivyohitajika.Labda kifaa kimoja kwa wanafunzi elfu.Je ,ilifaa kweli taasisi hii kuitwa chuo kikuu?Kule mesini pia chakula kiliuzwa kwa bei ghali.Haiyumkiniki mwanafunzi yoyote kuweza kuimudu bei ile isipokuwa wachache waliotoka kwenye aila za kimwinyi.Karo iliyolipwa haikulandana na huduma zilizotolewa sini!Huduma zilikuwa duni.Kingewezaje chuo hiki kuwa asai ya ufumbuzi wa kutatua matatizo halisia yaliyoikumba jamii ikiwa pembejeo muhimu hazikuwepo.Au ni kwa kuwa kilikuwa sehemu iliyotengwa sana na serikali?Au ni ule mtafaruku wa mdororo wa usalama?Kwa hilo sitetei katu.Visa vya utovu wa usalama vilituka kila uchao kawaida kama sheria.Vyuo vingine vya nchi ya Uzalendo vilikuwa tofauti kabisa.
Mbona mnyonge abaki kimya?Kumbe maudhi ndani ya nafsi hurundikana yakajenga joto na kulipuka moto mkubwa utishao!Basi wanagenzi wakaungana ili kulilia haki yao.Ila dau la mnyonge haliendi joshi.Taasisi kuu chuoni ikawaita hawa mabwana ''walinda usalama'' ili waje waulinde usalama.Nao waliulinda kweli.Kwa jinsi walivyowatambia wanafunzi waandamanaji hadithi ya kifimbo cheza na ile ya mtaka jamvi zote wakati mmoja.Walioathirika sana na dhuuluma hizi hasa walikuwa wanagenzi mabanati ambao wachache walinusurika tundu la sindano kutaka kunajisiwa na hao waliokujakuwalinda.Huu ndio usalama uliolindwa ;salama ulioimarishwa.
Na wimbo huu haunitoki ubongoni mwangu asilani hadi waleo.Ni sauti za wanyonge za vilio.
"Imefika,leo siku imefika,
Imefika,ya mabomu kulipuka,
Imefika,na haki itapatika,
Imefika,vikuku vitafunguka,
Imefika,ya mnyonge kutukuka,
Imefika,tena kutodhulumika,
Imefika,leo siku imefika. "
Walioandamana walifanya makosa kwa kuharibu mali ya chuo isiyokadirika.Walifunga maktaba,wakagoma kununua chakula bwalooni na hata kususia masomo hadi kilio chao kiliposikilizwa.Japo amani haiji ila kwa ncha ya upanga, mandamano yaliweza kuleta athari kubwa sana ya uharibifu wa mali.Walikuwa wakidai haki yao.Yalipangwa ya amani ila vichwa mchunga walianzisha vurumai.Hakuna mchele ukosao ndume na kila penye kundi la nzige na panzi wa papo.Kwa adhabu waliyopewa, walikubali matokeo .Hawakupinga ya wahenga kuwa yakija yapokee.La kuniatua ini bado ni lile la walinda usalama ambao walizidi kuitibua amani kwa kuendeleza dhuluma.Dhuluma ambayo kovu nilonalo sasa hunikumbusha ule wimbo wa mandamano.
Tulitoka nje ya chuo wakati jua likiaga miti wasaa wa magharibi.Tulipofika sitani mimi na Nusura tukapata basi la kwenda kwetu limashang'oa nanga.Mama yangu!Tungefanyanyaje katika hali ile.Hatukujua rafiki wala familia kule.Kiza kinene kikaanza kuifunika ardhi huku tukiwa tumejiinamia katika bahari ya mawazo tumbitumbi.
No comments:
Post a Comment